Pumzi ya Furaha

Pumzi ya Furaha

Lengo la somo hili ni…

Lengo la somo hili ni…

kusaidia kuamsha na kuendeleza nguvu mwilini mwako, na kuleta uhai katika pumzi na mwili wako. Zoezi hili husaidia kupunguza kupumua kwa juu juu kunakotokana na wasiwasi, kwa kuruhusu pumzi kujaza mapafu yote. “Pumzi ya Furaha” hutumia mwendo wa mwili wenye mpangilio na harakati za mikono zinazoendana na pumzi ili kukusaidia kudhibiti hisia zako, kuupa mwili nguvu, na kuamsha kila sehemu ya mwili.

Jinsi ya kujiandaa

Jinsi ya kujiandaa

Kabla ya kuanza…

Kusanya vifaa au nyenzo zako:

– chupa ya maji

– mkeka wa yoga au blanketi – ikiwa ungependa kusimama wakati wa kufanya zoezi hili, na/au kitu cha kukalia ikiwa ungependa kukaa (kiti kisicho na magurudumu)

– sehemu tambarare

Chagua mahali unapoipenda sana au panapokupa nguvu. Inaweza kuwa ndani au nje.
Unatakiwa uwe na chumba chenye kutosha kusonga, kuinama mbele, na kusogeza mikono juu, chini, na pembeni. Zoezi hili linaweza kurekebishwa na kufanya ukiwa umekaa.

Dhibiti usumbufu wako kadri uwezavyo:

Fikiria vitu vinavyokuharibia utulivu na jaribu kuvipunguza wakati huu. Zima vikumbukizi na taarifa kwenye simu yako ya mkononi na vifaa vingine; Wataarifu watu kuwa unahitaji muda kwa ajili ya zoezi hili; Funga mlango wako, n.k.

Tungependa kukukumbusha kwamba kama kuna kelele au kitu chochote kinachokukengeusha, iwe kutoka nje au ndani, tunakualika urejee katika sasa na uendelee kujitambua pamoja na mwendelezo wa zoezi hili.

Zoezi au shughuli

Zoezi au shughuli

Unapojisikia uko tayari kuanza…

Jiweke katika hali ya utulivu:

  • Vuta pumzi chache za kina,kwa ndani,kwa kuvuta ndani na nje.
  • Tafuta mahali pazuri pa kukaa, kulala chini, au kufanya kile kinachokufanya ujisikie vizuri zaidi.
  • Jikumbushe kuwa chochote kitakachotokea katika muda huu ni cha kuheshimika na ni sawa.

– Vuta pumzi chache za kina,kwa ndani,kwa kuvuta ndani na nje.

– Tafuta mahali pazuri pa kukaa, kulala chini, au kufanya kile kinachokufanya ujisikie vizuri zaidi.

Jikumbushe kuwa chochote kitakachotokea katika muda huu ni cha kuheshimika na ni sawa.

TAHADHARI

Survivor’s Sanctuary hutoa mazoezi ya mwendo kwa madhumuni ya elimu tu, na hayakusudiwi kuchukua nafasi ya ushauri, matibabu, au uchunguzi wa mtaalamu wa afya.
Ikiwa utahisi kizunguzungu, kuishiwa nguvu, kupumua kwa shida, au maumivu ya mwili unapofanya mazoezi, tafadhali simama mara moja na wasiliana na mtaalamu wa afya.

me too. International haina leseni kutoa huduma za afya.

Unakubali kuwa unabeba jukumu lote unapochagua kufanya mazoezi yoyote ya mwendo yaliyomo katika Survivor’s Sanctuary.

  • Ikiwa una shinikizo la damu la juu lisilotibiwa au una majeraha ya kichwa (kama kuumwa na kichwa sana au glaukoma), zoezi hili halipendekezwi kwako kwa sasa.
  • Ikiwa una shinikizo la damu la chini, fanya zoezi taratibu na usiiname sana.
  • Ikiwa una matatizo ya mgongo wa chini, bado unaweza kutumia mbinu hii lakini punguza mwendo wan katikati ya mwili na fanya kwa mwendo wa pole.
  • Tambua mipaka ya mwendo wa mikono na mabega yako, na usipite mpaka wako. Ingawa unaweza kuhisi kuvutika kadri unavyorudia harakati za mikono, zoezi hili halipaswi kukuumiza mikono au mabega.

Muda wa kutuliza au wa kuanza upya

Muda wa kutuliza au wa kuanza upya

Baada ya kukamilisha marudio ambayo yanakufanya ujisikie vizuri, simama kwa muda mfupi ukiwa na mikono yako imetulia au imening’inia pembeni. Kaa hapo hadi urudi kwenye mpangilio wako wa kawaida wa kupumua. Vuta pumzi kwa kina kupitia pua yako na toa pumzi yote kupitia mdomo. Funga macho yako na tambua athari za zoezi ulilofanya. Angalia kasi ya mapigo ya moyo wako; sikiliza hisia zilizo kwenye uso wako, mikono na viganja. Tafakari maswali haya: ni wapi unahisi uhai au mzunguko zaidi mwilini mwako? Ni wapi unahisi utulivu? Ubora wa mawazo yako ukoje? Hali yako ya hisia ikoje?

Mwaliko wa Kuunganisha

Ikiwa zoezi hili lilihisi vizuri kwako, tunakualika kufikiria jinsi unavyoweza kulijumuisha kwa makusudi zaidi katika maisha yako. Unaweza kujaribu kulifanya asubuhi kabla ya kuanza shughuli zako nyingine. Unaweza pia kulifanya mara kadhaa wakati wa siku unapojisikia mchovu au mwenye wasiwasi.

How would you rate this lesson?

Kadiria maudhui haya: