Kufanyia Kazi Vichocheo Vyako na Miitikio ya Mfumo wa Mishipa ya Fahamu

Kufanyia Kazi Vichocheo Vyako na Miitikio ya Mfumo wa Mishipa ya Fahamu

Nia ya somo hili ni…

Nia ya somo hili ni…

kuongeza uelewa wa jinsi mwili wako na mfumo mwitikio wa mfumo wa Neva unapochochewa. Iwe unalitambua jambo hili kwa makusudi au la, mwili wako huwa unatafuta usalama kila wakati. Unapojihusisha kwa makusudi katika mchakato wa kupona kutokana na uzoefu wa kiwewe au kidonda cha moyo/rohoni, unaweza kugundua kwamba chochote kinachoukumbusha mwili wako tukio la zamani la kiweweau jeraha huchukuliwa kama ishara ya hatari. Hali hii ndiyo tunayoita kichocheo.

album-art
00:00

Jinsi ya Kujiandaa

Jinsi ya Kujiandaa

Kabla hujaanza…

Kusanya vifaa au nyenzo zako:

– Karatasi moja (unaweza kutumia karatasi ya ukubwa wa 8.5 x 11, lakini inaweza pia kuwa ya ukubwa mwingine. Muhimu ni iweze kukunjwa katikati kwa urefu)

– Kitu cha kuandikia

Chagua eneo au mazingira unalojisikia huru na salama kujieleza.

Dhibiti usumbufu wakoi kadiri uwezavyo:

– Fikiria ni nini kawaida hukuvuruga na ujaribu kupunguza vishawishi hivyo wakati huu. Fikiria kuzima vikumbukuzi na taarifa kwenye vifaa vyako; waambie watu kuhusu muda unaohitaji kwa zoezi hili, funga mlango wako, n.k.

Tungependa kukukumbusha kwamba kama kuna kelele au kitu chochote kinachokukengeusha, iwe kutoka nje au ndani, tunakualika urejee katika sasa na uendelee kujitambua pamoja na mwendelezo wa zoezi hili.

Zoezi au shughuli

Zoezi au shughuli

Unapokua tayari kuanza…

Kua makini:

– Chukua pumzi chache za kina, ukiingiza na kutoa hewa polepole, ili kujituliza na kujihisi uko salama.
– Hupaswi kushiriki katika zoezi hili ikiwa kwa sasa umechochewa

Unapojisikia umetulia na uko salama, anza:

Kumbukumbu fupi kuhusu vichocheo:

  • Kichocheo ni mtazamo wa mwili wako kwamba kuna hatari katika mazingira yako. Vichocheo vinaweza kuhusiana na hali yetu ya kimwili au kihisia. Huenda kikawa ni kitu tulichowahi kuhisi hapo awali, kama vile hisia ya tumbo kusinyaa au hofu. Vichocheo vinaweza kuwa watu, maeneo, sauti, harufu au picha. Baadhi ya vichocheo huonekana kama vinatoka ndani yetu kupitia mawazo na hisia za mwilini.
  • Vichocheo vinaweza kujitokeza tunapokutana na hali iliyozoeleka, au kile tunachokitafsiri kuwa hali iliyozoeleka. Kichocheo si cha kimantiki; hutumia mantiki ya zamani kutatua changamoto mpya. Vichocheo pia ni vya kipekee kwa kila mtu na havipaswi kamwe kulinganishwa au kupuuzwa. Ingawa si mara zote inawezekana kuepuka kuchochewa, unaweza kujifunza jinsi ya kudhibiti mwitikio wako kwa kichocheo.

Chukua muda kuchunguza tukio moja la kichocheo kwako.


Katika zoezi hili, utachunguza tukio maalum ambapo ulichochewa na mwitikio wa mwili wako. Tafadhali chagua tukio (au matukio) ambayo unahisi yanaweza kushughulikiwa kwa usalama.

Anza kwa kukunja karatasi katikati kwa urefu.
Upande wa kushoto, orodhesha kichocheo/vichocheo; na upande wa kulia, andika miitikio ya mfumo wako wa neva. Unaweza kufanya hivi kwa tukio moja maalum la kichocheo au kupitia matukio machache na kutambua jinsi ulivyojibu katika kila hali.

Mfano:

Kichocheo: Mtu anafanya mzaha kuhusu unyanyasaji au ukatili wa kingono.
Mwitikio wa Mwili: Mapigo ya moyo yaliongezeka, nilihisi kichefuchefu tumboni, na nilihisi kama nataka kukimbia.

Kichocheo: Harufu ya chakula ambacho uliwahi kukipenda.
Mwitikio wa Mwili: Mabega yangu yanakuwa mazito na tumbo linaanza kugeuka.

  • Kutaja na kutambua vichocheo vyako kunaweza kukusaidia kudhibiti ukali wake. Kadri unavyozidi kuyafahamu maumbo ya hisia za mwilini zinazohusiana na kichocheo chako, ndivyo utakavyoweza kukikabili mapema zaidi. Kuwa mvumilivu katika kuchunguza na kutambua hisia za mwili wako; wakati mwingine huchukua muda kuunganika na hisia za mwilini.

Muda wa Kujituliza au wa kuanza upya

Muda wa Kujituliza au wa kuanza upya

Chukua muda mfupi upumue kwa utulivu na ujishukuru kwa kushiriki na kukamilisha shughuli hii.

Mwaliko wa kuunganishwa

Unapojitahidi kwa makusudi kudhibiti vichochezi vyako, unaweza kurudi kwenye karatasi hii mara kwa mara ili kuona jinsi mwitikio wa mfumo wako wa neva unavyobadilika kadri muda unavyopita.

How would you rate this lesson?

Kadiria maudhui haya: