Yoga

Yoga

Lengo la somo hili ni…

Lengo la somo hili ni…

kukutambulisha katika mila ya Asia Kusini ya yoga asana. Neno yoga linatokana na lugha ya Kisanskriti likimaanisha “kuunganisha” au “kuleta pamoja.” Mazoezi haya yanakualika kuunganisha pumzi, akili, na mwili. Yoga asana ni mkusanyiko wa harakati za kimwili zinazolenga kutuliza akili na kujenga nguvu pamoja na unyumbufu wa mwili.

Jinsi ya kujiandaa

Jinsi ya kujiandaa

Kabla ya kuanza…

Kusanya vifaa au nyenzo zako:

– Kunywa maji.

– Mkeka wa kufanyia mazoezi

–Maji

Chagua eneo halisi, ndani au nje ambapo unahisi kustarehesha na una nafasi ya kusonga kwa uhuru. Hakikisha una nafasi ya kutosha kunyoosha mikono yako kila upande bila kugonga kitu chochote.

Dhibiti usumbufu wako, kadri utakavyoweza.

Fikiria mambo ambayo huenda yatakayokuharibia utulivu na uyapunguze kadiri uwezavyo. Fikiria kuzima ukumbusho na arifa kwenye vifaa vyako; wajulishe watu muda unaohitaji kwa mazoezi haya, funga mlango wako. nk.
Tungependa kukukumbusha kwamba kama kuna kelele au kitu chochote kinachokukengeusha, iwe kutoka nje au ndani, tunakualika urejee katika sasa na uendelee kujitambua pamoja na mwendelezo wa zoezi hili.

Zoezi au shughuli

Zoezi au shughuli

Ukiwa tayari kuanza…

Kuwa makini:

– Kaa kwenye mkeka wako.

– Vuta pumzi chache kwa ndani na nje.

– Jikumbushe kwamba chochote kitakachojitokeza katika muda huu ni cha kuheshimika.

Ukiwa tayari, tazama video. Simamisha pale unapohitaji, na jipe ruhusa ya kusongesha kwa kasi yako mwenyewe.

TAARIFA MUHIMU

Survivor’s Sanctuary hutoa mazoezi ya mwendo yaliyoundwa kwa madhumuni ya kielimu pekee, na hayakusudiwi kuchukua nafasi ya ushauri, matibabu, au uchunguzi wa mtaalamu wa afya aliyeidhinishwa. Ikiwa utahisi kizunguzungu, kuzimia, upungufu wa pumzi, au usumbufu wa mwili wakati wa kusogea, tafadhali simama mara moja na wasiliana na mtaalamu wa afya.

me too. International haina leseni kutoa huduma za matibabu

Unakubali kuwajibika kikamilifu kwa maamuzi yako unapochagua kushiriki katika mazoezi yoyote ya mwendo yaliyo ndani ya Survivor’s Sanctuary.

Wakati wa kutuliza au wa kuanza upya

Wakati wa kutuliza au wa kuanza upya

Chukua muda kuhisi athari za mazoezi yako. Badilika kwa utaratibu kuelekea shughuli yako inayofuata.

Mwaliko wa Kuunganisha

Kama ulifurahia zoezi hili, lifanye tena mara nyingi kadiri unavyohitaji. Kama uliona mazoezi haya yakikuwa magumu, bila kuwa hatari, fikiria kurudia zoezi hili ukiwa katika hali tofauti ya mwili; angalia ni nini tofauti. Kama ulifurahia mazoezi, lifanye tena mara nyingi kadiri unavyohitaji. Fikiria jinsi unavyoweza kusitawisha mazoezi ya kutafakari kimakusudi. Je, ungependa kuongeza zoezi hili kwenye utaratibu wako wa asubuhi? je hili ni zoezi ambalo unarejea mwishoni mwa siku ndefu?

How would you rate this lesson?

Kadiria maudhui haya: