Toa Shukrani

Toa Shukrani

Lengo la somo hili ni…

Lengo la somo hili ni…

kukusaidia katika zoezi la kuonyesha shukrani – kwa kukusaidia kukumbuka na kutaja mambo unayotakiwa kushukurui.

Jinsi ya kujiandaa

How to prepare

Kabla ya kuanza…

Kusanya vifaa au nyenzo zako:

– daftari na vifaa vya kuandikia (ikiwa unataka)

– kifaa cha kurekodi sauti (ikiwa unataka)

– maji

Fikiria au chagua mahali katika mazingira yako unapopapenda sana au panapokupa nguvu. Inaweza kuwa ndani au nje.

Dhibiti usumbufu wako kadri uwezavyo:

– Fikiria vitu vvinavyokuharibia utulivu jaribu kuvipunguza wakati huu. Zima vikumbusho na arifa kwenye simu yako ya mkononi na vifaa vingine;Waambie watu kuwa unahitaji muda kwa ajili ya zoezi hili; Funga mlango wako, n.k.
Tungependa kukukumbusha kwamba kama kuna kelele au kitu chochote kinachokukengeusha, iwe kutoka nje au ndani, tunakualika urejee katika sasa na uendelee kujitambua pamoja na mwendelezo wa zoezi hili.

Zoezi au shughuli

Zoezi au shughuli

Unapojisikia uko tayari kuanza…

Jiweke katika hali ya utulivu:

– Pumua kwa ndani, vuta na kutoa hewa.

– Tafuta mahali pazuri pa kukaa au na ukae kwa namna unajojisikia ukiwa umestarehe

– Jikumbushe kuwa chochote kitakachotokea katika muda huu ni cha kuheshimika.

Kwa zoezi hii, utakamilisha kila sentensi kulingana na mwongozo uliotolewa. Unaweza kuandika, kurekodi sauti au video, kuchora au kufanya mchoro wa majibu yako. Jisikie huru kuongeza aina nyingine ya mwendo ikiwa itakufanya ujisikie vizuri.

Kabla ya kuanza, chukua muda kutambua hali ya mwili wako: ni hisia zipi zipo, na ni wapi unahisi mkazo au mvutano?

Unapoweka umakini wako kwenye kila jambo unalolishukuru, angalia kinachotokea mwilini mwako. Unapolifikiria jambo unalolishukuru, punguza mwendo na tambua hisia za mwili wako (mfano: mwendo, mvutano, au joto). Tambua jinsi shukrani inavyojisikia mwilini mwako. Unaweza pia kuandika au kurekodi haya uliyoyaona.

Maswali ya Shukrani:

  1. Ninashukuru kwa (mtu huyu)…
  2. Ninashukuru kwa (mahali hapa)…
  3. Ninashukuru kwa (fursa hii)…
  4. Ninashukuru kwa (funzo hili)…
  5. Ninashukuru kwa (matukio haya)…
  6. Ninashukuru kwa (kitu fulani kuhusu mimi mwenyewe).

Muda wa Kutuliza au kuanza upya

Muda wa Kutuliza au kuanza upya

Baada ya kumaliza maswali haya sita, rudisha umakini wako kwa makusudi kwenye mwili wako na tambua hali ya mwili wako sasa. Ni nini kilichobadilika tangu ulipoanza? Ni nini kimebaki kama kilivyokuwa?

Mwaliko wa Kuunganishwa

Ikiwa ulifurahia zoezi hili, rudi kulifanya mara nyingi kadri unavyohitaji. Fikiria kujumuisha zoezi la kila siku la shukrani katika maisha yako. Zoezi lako linaweza kuwa kutaja mambo kadhaa unayoyashukuru, au hata jambo moja tu. Fikiria kuunganisha zoezi la shukrani na jambo unalofanya kila siku (kama kupiga mswaki, kuoga, au kutengeneza chai) ili kuhakikisha unapata muda wa kulifanya zoezi hili.

How would you rate this lesson?

Kadiria maudhui haya: