5-4-3-2-1

5-4-3-2-1

Lengo la somo hili ni…

Lengo la somo hili ni…

kukusaidia kupata zana rahisi unapo hitaji utulivu wa akili au unapohitaji kujituliza. Zoezi hili hukuweka katika wakati wa sasa na huleta uelewa kwenye hisia zako. Limeundwa kukusaidia hasa katika nyakati za hisia juu.

album-art
00:00

Lengo la somo hili ni…

Lengo la somo hili ni…

kukusaidia kupata zana rahisi unapo hitaji utulivu wa akili au unapohitaji kujituliza. Zoezi hili hukuweka katika wakati wa sasa na huleta uelewa kwenye hisia zako. Limeundwa kukusaidia hasa katika nyakati za hisia juu.

album-art
00:00

Jinsi ya kujiandaa

Jinsi ya kujiandaa

Kabla ya kuanza…

Kusanya vifaa au nyenzo zako:

– kitu cha kujitutuliza (kama picha, taswira, kioo cha thamani au jiwe)

Chagua eneo – ndani au nje – ambalo unajisikia huru na salama, na lenye nafasi ya kutosha kujisogesha kwa urahisi.

Dhibiti vishawishi kadri uwezavyo:

– Fikiria mambo yanayokukengeusha mara nyingi na jaribu kuyapunguza wakati huu. Zima vikumbusho na arifa kwenye vifaa vyako; Waambie watu kuwa unahitaji muda kwa ajili ya zoezi hili,Funga mlango wako, n.k. Tungependa kukukumbusha kwamba kama kuna kelele au kitu chochote kinachokukengeusha, iwe kutoka nje au ndani, tunakualika urejee katika sasa na uendelee kujitambua pamoja na mwendelezo wa zoezi hili.

Zoezi au shughuli

Zoezi au shughuli

Unapohisi uko tayari kuanza…

Kua mtulivu:

– Pumua mara chache kwa kina, ingiza na kutoa hewa.

– Tafuta mkao unaokufanya ujihisi vizuri zaidi.

– Jikumbushe kuwa chochote kitakachotokea wakati huu ni cha heshima.

Kwa nini tunafanya zoezi la kupitia hisia tano?

Zoezi hili linaweza kutumiwa wakati wowote na mahali popote unapolihitaji. Unaweza kupitia hisia zako tano kwa kusema kwa sauti au kimya kimya moyoni mwako. Kutambua kwa makusudi kunasaidia kuutoa akili kwenye mawazo ya wasiwasi au yanayokusumbua, na hili husaidia kuleta utulivu mwilini.

  1. Tambua KITU Kimoja unachoweza kuonja. Ndani ya mdomo wako kuna ladha gani? Labda ni ladha ya peremende, chai au juisi.
  2. Tambua VITU viwili unavyoweza kunusa. Labda ni manukato yako, losheni, chakula ulichokula hivi karibuni, au leso unaolalia. Ukihitaji, unaweza kuchukua matembezi mafupi kutafuta harufu kama sabuni bafuni au harufu ya mazingira ya asili.
  3. Tambua VITU vitatu unavyoweza kusikia. Lenga sauti zilizo nje ya mwili wako, kama upepo wa feni au sauti ya saa, sauti za watoto walicheza. Ukisikia tumbo lako likinguruma, hilo pia linahesabika!
  4. Tambua VITU vinne unavyoweza kuhisi kimwili. Inaweza kuwa nguo zako, blanketi, au ardhi chini ya miguu yako.
  5. Tambua VITU vitano unavyoweza kuona karibu nawe. Inaweza kuwa kalamu, alama ukutani, kitu nje ya dirisha, au chochote kilicho karibu nawe sasa.

Wakati wa kutuliza au wa kuanza upya

Wakati wa kutuliza au wa kuanza upya

Pumua mara chache zaidi kwa kina kutoka tumboni ili kumaliza zoezi hili. Jitazame na uangalie hali yako ya hisia na ubora wa mawazo yako.

Katika nyakati za msongo au usumbufu, rudia zoezi hili kadri unavyohitaji.

Mwaliko wa kuunganishwa

Ikiwa umelihisi zoezi likiwa zuri, tunakualika utafakari jinsi unavyoweza kuwa makusudi katika kulijumuisha zaidi katika maisha yako. Kwa mfano, unaweza kupitia orodha ya 5-4-3-2-1 kabla ya kuongea mbele ya umati, au baada ya mazungumzo au mwingiliano wenye changamoto, au unapojaribu kutuliza akili yenye wasiwasi ili upumzike au ulale.

How would you rate this lesson?

Kadiria maudhui haya: