Tunastahili Furaha na Raha
Lengo la Somo Hili Ni…
Lengo la Somo Hili Ni…
kujikumusha kwamba tunastahili raha kuwa sehemu ya maisha yetu ya kila siku. Wakati mwingine simulizi huwa kwamba uponyaji unamaanisha tumekwama “kufanya kazi ngumu.” Zoezi hili linatualika kujiuliza: je, vipi kama uponyaji ungejisikia vizuri? Je, vipi kama uponyaji usingekuwa tu kushughulikia majeraha ya zamani bali pia kujihusisha na uzoefu wetu wa furaha na raha? Je, vipi kama mwendo usingekuwa tu wa kuachilia msongo bali pia wa kugundua raha ndani yetu wenyewe?
Jinsi ya kujiandaa
Zoezi au shughuli
Wakati wa Kujituliza au kuanza upya

Wakati wa Kujituliza au kuanza upya
Muda wako unapo kwisha, simama na vuta pumzi . Pumua ndani kupitia pua na nje kupitia mdomo na sauti kidogo mara 2-3. Tazama ilivyokuwa kufanya uchunguzi wa wazo la starehe. Chukua muda wako kujiheshimu kwa kutenga muda kwa shughuli hii, na ukumbushe nafsi yako kwamba unastahili starehe (unaweza kufanya hivyo kwa kujiambia kwa sauti).
Mwaliko wa Kuunganisha
Unakaribishwa kufikiria kuendelea na zoezi hili la raha kila siku kwa siku 7 zijazo. Unaweza kuweka shughuli ya kila siku kwenye kalenda yako kama ukumbusho. Ikiwa ungependa kufanya hivyo, kuwa mahsusi kuhusu shughuli utakayofanya, na fikiria baadhi ya mambo haya kimipango: Utafanyia wapi zoezi au shughuli hii? Utaifanya lini? Utaifanyaje? Inaweza kusaidia kumtambua rafiki au mshirika unayemwamini ambaye anaweza kukuulizia maendeleo yako na kuwa mshirika wako wa uwajibikaji kwa wiki hiyo. Unaweza kutumia muda sasa kufikiria ungependa mtu huyo awasiliane au ajihusishe nawe kwa namna gani. Kwa mfano, unaweza kumuomba akuulize kila siku kwa muda maalum ili kuona kama umekamilisha shughuli uliyokusudia kuifanya.
