Kuunda Jarida la Uponyaji

Kuunda Jarida la Uponyaji

Kusudi la somo hili ni…

Kusudi la somo hili ni…

kuunda kumbusho halisi la yale uliyojifunza na kukusanya katika safari yako ya uponyaji. Jarida hili ni fursa ya kuonyesha ubunifu wako na kukusanya kauli muhimu za kujikumbusha, uthibitisho chanya, nia, na ujumbe binafsi ambao unaweza kubeba pamoja nawe unapopitia katika ulimwengu.

album-art
00:00

Jinsi ya kujiandaa

Jinsi ya kujiandaa

Kabla ya kuanza…

Kusanya vifaa au nyenzo zako:

– Karatasi (ukurasa wa 8×11 utatosha vizuri)

– Kitu cha kuandika, kalamu za alama, penseli za rangi, au kalamu – chochote kinachoruhusu ubunifu wako uruke.

– Makasi & gundi

– Chaguo la kutumia magazeti ya zamani au kitabu cha picha

Chagua eneo ambalo unahisi huru kujieleza.

Dhibiti usumbufu wako, kadri utakavyoweza:

– Fikiria mambo ambayo huenda yakakusumbua/uharibifu utakaokuondolea utulivu na uyapunguze kadiri uwezavyo. Fikiria kuzima ukumbusho na arifa kwenye vifaa vyako; wajulishe watu muda unaohitaji kwa mazoezi haya, funga mlango wako. nk. Tungependa kukukumbusha kwamba kama kuna kelele au kitu chochote kinachokukengeusha, iwe kutoka nje au ndani, tunakualika urejee katika sasa na uendelee kujitambua pamoja na mwendelezo wa zoezi hili.

Zoezi au shughuli

Zoezi au shughuli

Unapohisi uko tayari kuanza…

Kuwa makini:

– Vuta pumzi chache za kina, ndani na nje.

– Ukumbushe nafsi yako kwamba chochote kitakachotokea wakati huu ni cha heshima.

Tuanze

  1. Weka nia kwa yale unayotaka kujumuisha katika jarida lako. Umealikwa kuwa na ubunifu na uchangamfu, au kuwa na msingi thabiti na fupi unavyopenda. Unaweza kuchagua kutumia jarida hili kama fursa ya kuchora au kuleta pamoja kwa picha maono yako ya maisha/dunia yatakavyokuwa katika siku zijazo, kushiriki manifesto/ilani yako ya uponyaji au barua ya kwako mwenyewe, kutumia kila ukurasa kuandika maneno yanakufanya uwe makini au maneno mazuri unayojiambia kimoyomoyo ama kwa sauti kama vile “Mimi ni wa maana”, kuandika shairi ya uponyaji au aina nyingine ya ushairi. Ni wewe kuamua nini utajumuisha katika kurasa hizi. Vuta pumzi chache kwa ndani na weka nia yako.
  2. Andaa Jarida! Utahitaji karatasi na makasi/ mkasi. Chukua karatasi yako na uikunje mara moja, mbili au tatu. Unapokunja karatasi zaidi, Jarida lako litaakuwa dogo na utakuwa na kurasa zaidi, unaweza pia kuongeza karatasi zaidi. Ukimaliza kukunja, kata pande zozote zilizounganishwa ili upande wa jarida umekujwa.
  3. Tumia muda kuunda na kujaza kurasa zako kulingana na nia uliyoweka awali. Jaribu kutofikiria sana kuhusu kuifanya iwe kamilifu kabisa. Hakuna mtu mwingine isipokuwa wewe utahitajii kuiona au kuishiriki nayo (ikiwa utachagua kuiweka iwe binafsi). Kwa hivyo, jaribu kadri utakavyoweza kuachilia shinikizo la kuiweka sawa kabisa kwa njia zote. Rudi kwenye pumzi yako unapohisi umeshikwa na mawazo kuhusu matokeo ya mwisho badala ya kuelezea unachotaka wakati huu.

Wakati wa kujituliza au kuanza upya

Wakati wa kujituliza au kuanza upya

Ukimaliza jarida yako (au ukiwa tayari kupumzika kutoka katika kuunda kwa sasa), chukua pumzi nyingine chache za kina. Pitia kurasa za kitabu ulichounda. Tambua nafsi yako kwa kupitia shughuli hii leo.

Mwaliko wa Kuunganisha

Unakaribishwa kutumia Jarida hii kwa namna utakavyoona inafaa. linaweza kubaki ndani ya begi unalobeba ili uweze kuitoa unapohitaji, au ukaweka mahali maalum ambapo unaweza kuichukua unapohitaji kujihisi umejikita katika maono yako ya uponyaji. Unaweza pia kufikiria kuunda jarida tofauti kwa mada au mahitaji maalum, na kujaribu kutumia mbinu na vifaa mbalimbali kutengeneza.

How would you rate this lesson?

Kadiria maudhui haya: