kukusaidia kukumbuka na kutekeleza shughuli na mazoea ya kiroho, kitamaduni na/au yanayohusiana na asili ambayo ungependa kuyajumuisha kwa makusudi katika safari yako ya uponyaji.
00:00
Jinsi ya kujiandaa
Jinsi ya kujiandaa
Kabla ya kuanza…
Kusanya vifaa au nyenzo zako:
– Kitu cha kugundulika (kama picha au sanamu, kristali au jiwe)
– Kinywaji unachope/nda
– Kitabu na karatasi
Chagua eneo unalohisi huru kujieleza.
Dhibiti usumbufu wako, kadiri utakavyoweza:
– Fikiria ni nini kinavyokuvuruga kwa kawaida na kupunguza usumbufu huo wakati huu. Fikiria kuzima ukumbusho na taarifa kwenye vifaa vyako; wajulisha watu wakati unahitaji kwa mazoezi haya, funga mlango wako. nk. Tungependa kukukumbusha kwamba kama kuna kelele au kitu chochote kinachokukengeusha, iwe kutoka nje au ndani, tunakualika urejee katika sasa na uendelee kujitambua pamoja na mwendelezo wa zoezi hili.
Zoezi au shughuli
Zoezi au shughuli
Unapohisi uko tayari kuanza…
Kuwa makini:
– Chukua pumzi chache za kina, ndani na nje.
– Ukumbushe nafsi yako kwamba chochote kitakachotokea wakati huu ni cha heshima.
Kuunda mazoezi ya mara kwa mara ya kiroho, kitamaduni na/au ya asili kunaweza kuunda nafasi salama kwako kutua unapoihitaji zaidi.
Sehemu ya 1: Jiachilie na Ukumbuke
Sehemu hii ya shughuli imeundwa kukusaidia kukumbuka na kufikiria mambo fulani yanayotegemea kiroho, yanayotegemea utamaduni na yanayotegemea asili, shughuli na/au mazoezi ambayo yameweza au yanaweza kukusaidia kwenye safari yako.
Kadri unavyojua zaidi kuhusu zana unazopata, ndivyo inavyokuwa rahisi zaidi kuziunganisha unapozihitaji.
Nini baadhi ya mambo, shughuli na/au desturi za kiroho unazokumbuka:
Zimekuweka imara?
Zinaendelea kukuimarisha?
Zingeweza kukuimarisha?
Mfano inaweza kuwa maombi/sala au ibada takatifu.
Mambo ya Kiroho
Shughuli za Kiroho
Matendo ya Kiroho
Zimekuimarisha
Zinakuimarisha
Zingeweza Kukuimarisha
Nini baadhi ya mambo, shughuli na/au desturi za kitamaduni unazokumbuka:
Zimekuimarisha?
Zinakuimarisha?
Zingeweza Kukuimarisha?
Mfano inaweza kuwa: sherehe (muziki, matukio ya kitamaduni, vyakula, n.k.).
Mambo ya Kitamaduni
Shughuli za Kitamaduni
Mara za Kitamaduni / Matendo ya Kitamaduni
Zimekuimarisha
Zinakuimarisha
Zingeweza Kukuimarisha
Nini baadhi ya mambo, shughuli na/au desturi zinazohusiana na asili unazokumbuka:
Zimekuimarisha?
Zinakuimarisha?
Zingeweza Kukuimarisha?
Mfano waweza kuwa: kutembea nje kila siku, kusikiliza sauti za ndege katika asili.
Vitu Vinavyotokana na Asili
Shughuli za Asili
Matendo ya Asili
Zimekuimarisha
Zinakuimarisha
Zingeweza Kukuimarisha
Sehemu ya 2: Kazia Fikira Jambo MOJA
Tambua mambo katika Sehemu ya 1 ambayo ungependa kuchunguza kwa undani zaidi na uandike orodha iliyofanyiwa marekebisho.
Chagua jambo moja katika orodha hiyo unalopaswa kukazia fikira, na ufikirie kwa nini uliamua kuchagua jambo hilo, au zoezi hilo.
Tafakari jinsi unaweza kuunganisha au kuboresha jambo hilo, utendaji au zoezi hilo katika maisha yako sasa.
Wakati wa Kujituliza au kuanza upya
Wakati wa Kujituliza au kuanza upya
Chukua muda kupumua au kuvuta pumzi na kujishukuru kwa kujiruhusu kukumbuka baadhi ya mambo, shughuli na mazoea yanayokuweka umejikita na thabiti.
Mwaliko wa Kuunganishwa
Fikiria jinsi unavyoweza kukuza mazoea ya makusudi ya kujumuisha mambo, shughuli na mazoea ya kiroho, kitamaduni na yanayohusiana na asili katika safari yako ya uponyaji. Je, ingekusaidia kuunda ratiba ya mara kwa mara ya kupitia upya orodha yako ya mazoea ya kiroho, kitamaduni na yanayohusiana na asili yanayokuunga mkono katika safari yako?
How would you rate this lesson?
Kuingia
Kufikia program hii kunahitaji kuingia. Tafadhali weka taarifa zako hapa chini!