Kuunda Mpango wa Kujirejesha Kwenye Utulivu

Kuunda Mpango wa Kujirejesha Kwenye Utulivu

Nia ya somo hili ni…

Nia ya somo hili ni…

Kukusaidia kuunda zana ambayo unaweza kutumia kukuza ustahimilivu wako. Kwa kuunda Hifadhi ya Zana, unaweza kuhakikisha kuwa una mikakati ya kupelekea ambayo utatumia kwa kupunguza mvutano na kutatua matatizo.

album-art
00:00

    Jinsi ya kujiandaa

    Jinsi ya kujiandaa

    Kabla ya kuanza…

    Kusanya vifaa au nyenzo zako:

    – Shajara, au mahali pa kurekodi mpango wako

    – kalamu

    – muziki wa kutuliza au harufu unazopenda kutumia kuimarisha nafasi yako

    Chagua mahali penye raha – ndani au nje – ambapo unahisi uhuru wa kujieleza.

    Dhibiti usumbufu wako, kadri utakavyoweza:

    – Fikiria ni nini hukukuvuruga mara nyingi na kupunguza usumbufu huo wakati huu. Fikiria kuzima ukumbusho na arifa kwenye vifaa vyako; wahabarisha watu wakati unahitaji kwa mazoezi haya, funga mlango wako. nk. Tungependa kukukumbusha kwamba kama kuna kelele au kitu chochote kinachokukengeusha, iwe kutoka nje au ndani, tunakualika urejee katika sasa na uendelee kujitambua pamoja na mwendelezo wa zoezi hili.

    Zoezi au shughuli

    Zoezi au shughuli

    Unapohisi uko tayari kuanza…

    Kuwa makini:

    – Vuta pumzi chache za kina na kutoa nje.

    – Elekeza ufahamu wako kwenye mwili wako, kisha tambua jinsi unavyohisi kihisia kwa wakati huu. Zingatia hali ya mawazo yako na hisia zozote unazozipata ndani ya mwili wako au katika mazingira yanayokuzunguka

    – Ukumbushe nafsi yako kwamba chochote kitakachotokea wakati huu ni cha kuheshimika.

    Kwa Nini Tunaunda Mpango wa Kujituliza?

    Mazoezi haya yamekusudiwa kukusaidia kurejea katika hali yako ya utulivu na kujidhibiti. Mpango huu unakuhimiza kuongeza ufahamu wa mahitaji yako ili uweze kutumia mbinu zinazokusaidia kurejea katika hali ya utulivu kabla hujafadhaika kiasi cha kupoteza udhibiti wa mawazo na tabia zako

    Tuanze

    • Anza kwa kutafakari mambo ambayo kwa kawaida unayatambua unapohisi umefadhaika. Ni hisia zipi au ishara zipi za tahadhari unazoziona ndani yako? Andika sehemu ya kwanza ya mpango wako kwa kichwa cha habari, “Ishara Zangu.” Chukua muda kujijibu maswali haya: Ni hisia zipi za kimwili zinazokujulisha kuwa unaanza kuhisi hasira au huzuni? Ni mawazo au mitazamo ipi inayojitokeza mara nyingi unapokuwa na hasira au unapohisi umelemewa? Kwenye ukurasa wa kwanza au sehemu ya kwanza ya karatasi yako, andika baadhi ya ishara hizo.
    • Kisha, andika kichwa cha habari cha sehemu inayofuata: “Mfumo Wangu wa Usaidizi.” Katika sehemu hii, chukua muda kutambua watu na maeneo yanayokupa msaada unapohisi umefadhaika. Unaalikwa kufikiria na kuandika majina ya watu watatu pamoja na njia za kuwasiliana nao ambao unaweza kuwajumuisha katika mtandao wako wa usaidizi. Watu hawa wanaweza kukupa uwepo wa kujali na kukusikiliza au kukusaidia kupitia hisia au hali ngumu. Unaweza pia kuandika sehemu chache zinazokusaidia kujituliza unapohitaji kujidhibiti. Huenda ikawa bustani ya karibu, mti unaoupenda, au sehemu maalumu katika ua wa nyumbani kwako.
    • Sehemu inayofuata ni “Orodha Yangu ya Mbinu za Kujitunza.” Ni mambo gani unayoweza kufanya ili kujituliza na kujisaidia kurejea katika hali ya utulivu? Ni vyema kuorodhesha hapa hatua rahisi unazoweza kuchukua bila kuongeza msongo wa mawazo kwa kuhitaji maandalizi au juhudi nyingi.
      • Baadhi ya mifano ya mbinu za kukabiliana na hali ngumu unazoweza kutumia unapohitaji kujitunza ni: kutembea, kuhesabu kurudi nyuma kuanzia 10, kujiweka mbali na mtu au hali inayokukera, kutenga muda wa kushiriki shughuli za burudani zisizo za ushindani, kusoma au kusikiliza muziki, kupitisha mkono wako chini ya maji baridi, kujimwagia maji baridi usoni, na kufanya zoezi la Mng’ono na Kujitikisa.
    • Sehemu ya mwisho ya mpango wako iwe na kauli moja ya kujithibitisha inayokukumbusha kurejea katika hali ya utulivu. Hii inaweza kuwa kauli unayoweza kusoma au kujisemea kwa sauti kama ukumbusho wa lengo lako la uponyaji, au maneno machache yanayokusaidia kurejea katika hali yako ya utulivu.

    Wakati wa kutuliza au kuanza upya

    Wakati wa kutuliza au kuanza upya

    Chukua pumzi chache za kina na kutoa nje. Shukuru nafsi yako kwa kumaliza zoezi hili leo.

    Mwaliko wa Kuunganishwa

    Unaweza kuchagua kuweka Hifadhi ya Zana mahali utaweza kuipata nyakati unahitaji kurudia mazoezi haya.

    How would you rate this lesson?

    Rate this content:
    Let us suggest a lesson.
    Let us suggest a lesson