Namna ya Kukuza Mazoea ya Shukrani

Namna ya Kukuza Mazoea ya Shukrani

Lengo la somo hili ni…

Lengo la somo hili ni…

kukusaidia kuelewa shukrani ni nini, kukupa nafasi ya kupata wakati wa kushukuru, na kukusaidia kufikiria jinsi unavyoweza kukuza kukuza tabia yako ya shukran.

album-art
00:00

    Jinsi ya kujiandaa

    Jinsi ya kujiandaa

    Kabla ya kuanza…

    Kusanya vifaa au nyenzo zako.

    • Kitu cha kuandikia na kifaa cha kuandikia.
    • Tumia simu au kifaa chako ukirekodi sauti yako (kwa hiari )
      Chagua mazingira mazuri unayoyapenda(yenye kuleta shukrani) na pata mkao wa mwili unaokupa utulivu (unaweza kusimama au kukaa).

    Chagua mazingira mazuri unayoyapenda(yenye kuleta shukrani) na pata mkao wa mwili unaokupa utulivu (unaweza kusimama au kukaa).

    Dhibiti usumbufu wako kadiri unavyoweza:

    • Fikiria mambo ambayo huenda yakakusumbua na uyapunguze kadiri uwezavyo. Fikiria kuzima ukumbusho na taarifa kwenye vifaa au nyenzo zako; wajulishe watu muda unaohitaji kwa mazoezi haya, funga mlango wako. nk. Tungependa kukukumbusha kwamba kama kuna kelele au kitu chochote kinachokukengeusha, iwe kutoka nje au ndani, tunakualika urejee katika sasa na uendelee kujitambua pamoja na mwendelezo wa zoezi hili

    Zoezi au shughuli

    Zoezi au shughuli

    Unapohisi uko tayari kuanza…

    Kuwa makini:

    • Pumua kwa kina mara kadhaa,ukivuta hewa ndani na nje.
    • Jikumbushe kwamba chochote kitakachotokea wakati huu ni cha heshima na kinakubalika.

    Kwa nini tunatoa shukrani?

    “Shukrani ni kuwa na shukrani moyoni na kuonyesha kuthamini. Kukuza mazoea ya shukrani ni muhimu katika safari yako ya uponyaji na hukusaidia kuona mema yaliyopo katika maisha yako. Kadri unavyotambua mema katika maisha yako, ndivyo mema hayo yanavyozidi kuongezeka. Mazoea ya shukrani hukusaidia kutambua ni nani na nini kinaleta mema katika maisha yako na hukuhimiza kutoa shukrani kwa yale unayoyathamini.”

    Tumia muda kufikiria swali lifuatalo:

    “Ninashukuru kwa…”

    Kumbuka kwamba hakuna jambo lililo dogo sana lisilostahili kutambuliwa.

    Muda wa kutuliza au wa kuanza upya

    Muda wa kutuliza au wa kuanza upya

    Chukua muda mfupi kupumua na ujishukuru kwa kushiriki katika zoiezi au shughuli hii.

    Mwaliko wa kuunganishwa

    Fikiria jinsi unavyoweza kukuza mazoea ya shukrani kwa makusudi. Kwa mfano, jibu swali: “Ninashukuru kwa nini, kwa sasa?” na tengeneza orodha ya nyimbo za shukrani, kopo la shukrani, bango la maono ya shukrani, au fanya jambo lingine lolote linalokuhamasisha kutoa shukrani.

    How would you rate this lesson?

    Rate this content:
    Let us suggest a lesson.
    Let us suggest a lesson