Qigong

Qigong

Lengo ya somo hili ni…

Lengo ya somo hili ni…

kukutambulisha mazoezi ya tiba ya Kichina ya qigong, pia inaitwa chi gong au qi gong. Mazoezi haya ya nishati yanajumuisha nafasi za mwili zilizoratibiwa, mwendo, kupumua, na kutafakari zinazotumiwa kwa madhumuni ya kuboresha afya yako. Qigong inasaidia kusogeza nishati iliyokwama na isiyosonga mwilini.

Jinsi ya kujiandaa

Jinsi ya kujiandaa

Kusanya vifaa au nyenzo zako:

– Mkeka wa kufanya mazoezi

– Maji

Chagua eneo unalohisi lenye kustarehesha kulisogelea. Hakikisha una nafasi ya kutosha ya kulala chini na kunyosha mikono yako kwa mlalo na kwa wima, bila kugonga chochote.

Dhibiti usumbufu wako, kadri utakavyoweza kwa:

Fikiria mambo ambayo huenda yatakuletea uharibifu au kukukosesha utulivu na uyapunguze kadiri uwezavyo. Fikiria kuzima ukumbusho na arifa kwenye vifaa vyako; wajulishe watu muda unaohitaji kwa mazoezi haya, funga mlango wako. nk.

Tungependa kukukumbusha kwamba kama kuna kelele au kitu chochote kinachokukengeusha, iwe kutoka nje au ndani, tunakualika urejee katika sasa na uendelee kujitambua pamoja na mwendelezo wa zoezi hili.

Zoezi au shughuli

Zoezi au shughuli

Unapohisi uko tayari kuanza…

Kuwa makini:

– Kaa kwenye mkeka wako.

– Vuta pumzi chache za kina na kutoa nje.

– Ukumbushe nafsi yako kwamba chochote kitakachotokea wakati huu ni chenye kuheshimika.

Ukiwa tayari, tazama video. Simamisha unapohitaji, na uipe nafsi yako ruhusa ya kusonga kwa kasi yako mwenyewe.

TAHADHARI

Survivor’s Sanctuary hutoa mazoezi ya mwendo yaliyoundwa kwa madhumuni ya kielimu pekee, na hayakusudiwi kuchukua nafasi ya ushauri, matibabu, au uchunguzi wa mtaalamu wa afya aliyeidhinishwa. Ikiwa utahisi kizunguzungu, kuzimia, upungufu wa pumzi, au usumbufu wa mwili wakati wa kusogea, tafadhali simama mara moja na wasiliana na mtaalamu wa afya.

me too. International haina leseni ya kutoa kutoa huduma ya matibabu.

Unakubali kuwa unachukua wajibu wote unapochagua kutenda kwa mazoezi yoyote ya mwendo yaliyomo kwenye Survivor’s Sanctuary.

Wakati wa Kutuliza au wa kuanza upya

Wakati wa Kutuliza au wa kuanza upya

Chukua muda kuhisi athari za mazoezi yako. Badilika taratibu kuelekea shughuli yako inayofuata.

Mwaliko wa Kuunganisha

Ikiwa umefurahia zoezi hili, rudi kulifanya mara nyingi kadri unavyohitaji/unavyoweza. Ikiwa uliliona kuwa la changamoto, bila kuwa na madhara, fikiria kulirudia ukiwa katika hali tofauti ya mwili; tambua kilicho tofauti. Fikiria jinsi unavyoweza kukuza mazoea ya makusudi ya Qigong. Je, ungependa kuliongeza katika utaratibu wako wa asubuhi? Au ni zoezi ambalo unaweza kulirudia mwishoni mwa siku ndefu au siku yenye mambo mengi?

How would you rate this lesson?

Kadiria maudhui haya: