Mwongozo wa Kutafakari Kuhusu Hatia na Aibu

Mwongozo wa Kutafakari Kuhusu Hatia na Aibu

Lengo la somo hili ni…

Lengo la somo hili ni…

kuchunguza hisia zako za hatia na/au aibu. Zoezi hii ni mwaliko wa kutoa sauti kwa hisia au uzoefu ambao mara nyingi hubaki umefichwa (kutoka kwa wengine na hata kwetu wenyewe). Inaweza kuwa na manufaa kwako kupitia shughuli hii ikiwa una nia ya kuchunguza kile ambacho hatia na aibu zako zinataka kusema au kukufundisha katika wakati huu.

album-art
00:00

Jinsi ya kujiandaa

Jinsi ya kujiandaa

Kabla ya kuanza…

Kusanya vifaa au nyenzo zako:

  • daftari
  • vifaa au nyenzo za kuandikia
  • maji

Chagua eneo ambalo unajisikia huru na salama kujieleza.

Dhibiti usumbufu wako kadri uwezavyo:

  • Fikiria mambo yanayokusumbua mara nyingi na jaribu kuyapunguza wakati huu. Zima vikumbusho na arifa kwenye simu yako ya mkononi na vifaa vingine;Waambie watu kuwa unahitaji muda kwa ajili ya zoezi hili; Funga mlango wako, n.k. Tungependa kukukumbusha kwamba kama kuna kelele au kitu chochote kinachokukengeusha, iwe kutoka nje au ndani, tunakualika urejee katika sasa na uendelee kujitambua pamoja na mwendelezo wa zoezi hili.

Zoezi au shughuli

Zoezi au shughuli

Unapohisi uko tayari kuanza…

Kuwa makini:

  • Vuta pumzi ndefu mara chache ndani na nje.
  • Jikumbushe kuwa chochote kitakachojitokeza wakati huu ni cha heshima na kinakubalika.
  • Tambua na ukubali hali yako ya sasa. Unajisikiaje? Ni hisia au mihemko gani ipo mwilini mwako kwa sasa?

Tuanze

Katika shughuli hii, unaalikwa kuandika barua kama mazungumzo kati yako na sehemu ya ndani yako inayohisi hatia au aibu.

  • Kabla ya kuanza kuandika barua, inaweza kukusaidia kuchukua dakika chache kufikiria ni uzoefu gani ungependa kuchunguza zaidi katika shughuli hii. Unaweza kuanza kwa kutafakari wakati ambao uliwahi kujisikia na hatia au aibu. Huu unaweza kuwa tukio la hivi karibuni, au uzoefu wa zamani ambao uliwahi kupitia.
  • Angalia kama uko tayari kuanza kuandika barua sasa, au kama unahitaji muda zaidi kujenga muktadha wako binafsi na uelewa wa kile unachoandika. Inaweza kusaidia kutumia muda kuelezea jinsi hatia au aibu yako inavyoonekana na inavyohisiwa. Unaweza kufanya hivi kwa kutafakari maswali yafuatayo, kuyaandika majibu yako, au kuyazungumza (kwako mwenyewe au kwa kurekodi sauti):
    • Ungelipa jina gani hatia au aibu yako?
    • Hatia au aibu yako ina umri gani?
    • Inaonekanaje? Inavaa nini?
    • Inakukumbusha mtu fulani katika maisha yako? Au inakukumbusha wewe katika umri fulani au kipindi fulani cha maisha yako?
    • Kwa nini unaamini wanahisi hatia au aibu? Je, kuna tukio maalum lililosababisha hisia hizi?
  • Baada ya kutafakari baadhi ya maswali haya, unaalikwa kuanza kuandika barua yako. Kuna njia mbili kuu za kuandika barua hii: 1, Unaweza kuandika kwa hatia au aibu yako kutoka katika mtazamo wako kama mtu aliyepitia uzoefu huo, au 2. Unaweza kujiandikia wewe mwenyewe kutoka mtazamo wa hatia au aibu yako. Unaweza kuanza kwa: “Mpendwa Hatia/Aibu…” au “Mpendwa [Jina lako]…”

Barua yako ikikamilika…

  • Isaini (iwe ni kutoka kwa hatia/aibu yako au kutoka kwako mwenyewe). Vuta pumzi ndefu chache, zikija kutoka tumboni. Tumia muda huu kutambua hali ya hisia au mihemko iliyo mwilini mwako sasa. Ni nini kimebadilika tangu uanze shughuli hii? Ni nini bado kipo?

Muda wa kutuliza au kuanza upya

Muda wa kutuliza au kuanza upya

Utaamua ungependa kufanya nini na barua uliyoandika. Je, ungependa kuihifadhi au kuiachilia au kuitupa? Baadhi ya chaguo unayoalikwa kuyazingatia ni: unaweza kuiweka kwenye bahasha au kwenye shajara ili uisome tena wakati mwingine katika siku zijazo; unaweza kuirarua au kuichoma; unaweza kwenda mtoni au kwenye maji mengine na kuiachia huko; au kuitupa kwa njia nyingine yoyote unayoihisi inakufaa. Kulingana na kile kilichojitokeza wakati wa kuandika, unaweza pia kuamua kusoma barua hiyo na mtu unayemuamini.

Mwaliko wa kuunganisha

Tunapoangazia hatia na aibu zetu, kwa kweli tunarejesha nguvu zetu. Lengo si kuacha kabisa kuhisi hisia hizi, kwa sababu zinaweza kuwa na mchango mzuri katika mahusiano yetu na wengine. Badala yake, ni muhimu zaidi kufanya kazi ya kutohisi hisia hizi kuhusu uzoefu, nyakati au tabia zinazotufanya tuhisi wadogo na waoga. Inaweza kukutuliza kujumuisha hili zoezi la kuongea na hisia zako ili kutoa yaliyokwama moyoni mwako au kuandika barua hizi ili kuelewa chanzo na muundo wa hisia zako za hatia, aibu, hasira, majuto au kuchanganyikiwa.

How would you rate this lesson?

Kadiria maudhui haya: