Zoezi au shughuli
Unapohisi uko tayari kuanza…
Kua makini:
– Vuta pumzi chache ndefu ndani na nje.
– Jikumbushe kwamba chochote kitakachojitokeza wakati huu ni cha heshima na kinastahili.
Kwa nini tunafanya mazoezi ya mazungumzo chanya ya kujithibitisha?
Zoezi hii inakupa nafasi ya kuchunguza na kutambua maneno unayotumia kuzungumza kuhusu wewe mwenyewe, wengine, na ulimwengu unaokuzunguka. Njia unavyozungumza na wewe mwenyewe, kuhusu wewe mwenyewe, ni kielelezo cha jinsi unavyojiona kwa sasa.
Tunaelewa kuwa hili linaweza kuwa eneo gumu kulifanyia kazi; hivyo, jitunze unapohitaji na uwe mvumilivu kwako mwenyewe.
Washa muziki wako na anza kufanya mazoezi yafuatayo.
Sehemu ya 1: Mahusiano
- Tazama orodha iliyo hapa chini, na utambue tu kinachotokea akilini na mwilini mwako unapopitia maneno haya. Usifanye chochote.
Maneno 8
- Kujitambua na Kujikubali
- Mipaka binafsi
- Huruma binafsi
- Ubunifu binafsi
- Furaha binafsi
- Amani binafsi
- Raha binafsi
- Kujiamini
- Andika kila neno.
- Andika kile kinachokujia akilini unapojifikiria mwenyewe kuhusiana na kila neno.
- Chora duara nje ya neno moja kwenye orodha ambalo linajitokeza zaidi kwako.
- Tafakari neno ulilozungushia duara, kisha andika kile unachogundua na chochote kinachojitokeza kwako.
- Tafakari eneo au maeneo ya maisha yako ambayo yangefaidika iwapo ungeongeza zaidi maana ya neno hilo.
Sehemu ya 2: Chupa ya Uthibitisho wa Nafsi
- Taja mambo kumi (10) mzuri unayoamini kuhusu wewe mwenyewe. Fikiria mambo mazuri ambayo rafiki au mtu unayempenda angesema kukuhusu. Kwa mfano: tabasamu lako, ucheshi wako, kujitolea kwako kusaidia wengine, n.k. Kumbuka, hakuna sifa iliyo ndogo sana!
- Kata angalau vipande vidogo 10 vya karatasi na uandike sifa moja mzuri kwenye kila kipande.
- Kunja kila uthibitisho (affirmation) na uviweke ndani ya chupa yako.
Unapoendelea na safari yako ya uponyaji, endelea kuongeza karatasi mpya kwenye chupa yako kadri unavyogundua mambo zaidi unayotaka kujithamini nayo—na chukua karatasi kutoka kwenye chupa yako mara kwa mara ili kujikumbusha.