Mapumziko matakatifu

Mapumziko matakatifu

Lengo la somo hili ni…

Lengo la somo hili ni…

kukusaidia kufafanua mapumziko kwa ajili yako mwenyewe; kufanya mazoezi ya kupumzika; kutathmini na kutafakari ulipo katika safari yako ya mapumziko; na kutaja kile utakachohitaji kujumuisha ili kuheshimu mazoea yako ya kupumzika.

album-art
00:00

Jinsi ya kujiandaa

Jinsi ya kujiandaa

Kabla ya Kuanza…

Kusanya vifaa au nyenzo zako:

– Kitu cha kukuweka katika utulivu (kama picha au taswira, kioo cha madini au jiwe)

– Kinywaji chako unachokipenda

Chagua sehemu ambapo unajisikia huru kupumzisha akili na mwili wako, pamoja na kupokea taarifa.

Dhibiti usumbufu wako, kadri utakavyoweza:

Fikiria mambo ambayo huenda yakakusumbua na uyapunguze kadiri uwezavyo. Fikiria kuzima ukumbusho na arifa kwenye vifaa vyako; wajulishe watu muda unaohitaji kwa mazoezi haya, funga mlango wako. nk. Tungependa kukukumbusha kwamba kama kuna kelele au kitu chochote kinachokukengeusha, iwe kutoka nje au ndani, tunakualika urejee katika sasa na uendelee kujitambua pamoja na mwendelezo wa zoezi hili.

Zoezi au shughuli

Zoezi au shughuli

Ukiwa tayari kuanza…

Kuwa makini:

– Vuta pumzi chache ndani na nje.

– Tafuta mkao unaokufanya ujisikie vizuri zaidi.

– Jikumbushe kwamba chochote kitakachojitokeza katika muda huu ni cha kuheshimika.

Kwa Nini Tunafanya Mazoezi ya Mapumziko Matakatifu?

Mapumziko ni sehemu muhimu ya ustawi wako wa jumla na safari yako ya uponyaji.

Mapumziko yanajumuisha tabia na shughuli zinazolenga kuongeza ustawi wako wa kimwili na kiakili, na mara nyingi huhusisha kusimamisha shughuli fulani. Mapumziko hukusaidia kupona kutokana na juhudi za kimwili na kiakili, na yanahusisha mambo kama mazoezi ya umakinifu yanayoimarisha uwezo wako wa kuwa na kubaki katika hali ya uwepo na akili yako, mwili, roho, na ulimwengu mpana unaokuzunguka.

Mazoezi yafuatayo yameundwa kukusaidia kufafanua mapumziko kwa ajili yako mwenyewe, kufanya mazoezi ya kupumzika, kutathmini ulipo katika safari yako ya mapumziko, na kutaja kile utakachohitaji kufanya ili kuweza kuheshimu mazoezi haya mara kwa mara.

Zoezi la 1: Fafanua Mapumziko

  • Mapumziko ni nini kwako?
    • Yanahisika vipi?
    • Yanasikika vipi?
    • Yanaonekana vipi?

Zoezi la 2: Fanya Mazoezi ya Kupumzika

Kwa kuzingatia ufafanuzi wako, acha kuandika na kaa tu na wewe mwenyewe pamoja na yale uliyofafanua.

Usifanye chochote, na jipe nafasi na muda kadiri unavyohitaji ili kuheshimu mapumziko sasa.

Ukiwa umekaa na wewe mwenyewe:

  • Sikiliza.
  • Pumua/vuta pumzi.
  • Shiriki (na wewe mwenyewe).
  • Ruhusu.
  • Achilia.
  • Rudia.

Zoezi la 3: Tafakari Uzoefu Wako wa Kupumzika

  • Umejifunza nini?
  • Umejifunza nini kuhusu wewe mwenyewe na mapumziko?
  • Je, utabadilishaje ufafanuzi wako kutoka Zoezi la 1 sasa?
  • Ni nini utaanza kujumuisha katika mazoezi yako ya mapumziko kuanzia sasa?

Wakati wa kutuliza au wa kuanza upya

Wakati wa kutuliza au wa kuanza upya

Chukua muda pumua au kuvuta pumzi na kujishukuru kwa kushiriki katika shughuli hii.

Mwaliko wa Kuunganisha

Fikiria jinsi unavyoweza kuendeleza mazoea ya makusudi ya mapumziko katika maisha yako. Ni hatua ipi ya kwanza unaweza kuanza nayo?

How would you rate this lesson?

Kadiria maudhui haya: