Zoezi au shughuli
Unapokua tayari kuanza…
Kua makini:
- Chukua pumzi chache za kina, ukiingiza na kutoa hewa polepole, ili kujituliza na kujihisi uko salama.
- Hupaswi kushiriki katika zoezi hili ikiwa kwa sasa umechochewa.
Unapojisikia umetulia na uko salama, anza:
- Kumbukumbu fupi kuhusu vichocheo:
- Kichocheo ni mtazamo wa mwili wako kwamba kuna hatari katika mazingira yako. Vichocheo vinaweza kuhusiana na hali yetu ya kimwili au kihisia. Huenda kikawa ni kitu tulichowahi kuhisi hapo awali, kama vile hisia ya tumbo kusinyaa au hofu. Vichocheo vinaweza kuwa watu, maeneo, sauti, harufu au picha. Baadhi ya vichocheo huonekana kama vinatoka ndani yetu kupitia mawazo na hisia za mwilini.
- Vichocheo vinaweza kujitokeza tunapokutana na hali iliyozoeleka, au kile tunachokitafsiri kuwa hali iliyozoeleka. Kichocheo si cha kimantiki; hutumia mantiki ya zamani kutatua changamoto mpya. Vichocheo pia ni vya kipekee kwa kila mtu na havipaswi kamwe kulinganishwa au kupuuzwa. Ingawa si mara zote inawezekana kuepuka kuchochewa, unaweza kujifunza jinsi ya kudhibiti mwitikio wako kwa kichocheo.
- Chukua muda kuchunguza tukio moja la kichocheo kwako.
- Katika zoezi hili, utachunguza tukio maalum ambapo ulichochewa na mwitikio wa mwili wako. Tafadhali chagua tukio (au matukio) ambayo unahisi yanaweza kushughulikiwa kwa usalama.
- Anza kwa kukunja karatasi katikati kwa urefu.
- Upande wa kushoto, orodhesha kichocheo/vichocheo; na upande wa kulia, andika miitikio ya mfumo wako wa neva. Unaweza kufanya hivi kwa tukio moja maalum la kichocheo au kupitia matukio machache na kutambua jinsi ulivyojibu katika kila hali.
Mfano:
Kichocheo: Mtu anafanya mzaha kuhusu unyanyasaji au ukatili wa kingono. Mwitikio wa Mwili: Mapigo ya moyo yaliongezeka, nilihisi kichefuchefu tumboni, na nilihisi kama nataka kukimbia.
Kichocheo: Harufu ya chakula ambacho uliwahi kukipenda. Mwitikio wa Mwili: Mabega yangu yanakuwa mazito na tumbo linaanza kugeuka.
- Kutaja na kutambua vichocheo vyako kunaweza kukusaidia kudhibiti ukali wake. Kadri unavyozidi kuyafahamu maumbo ya hisia za mwilini zinazohusiana na kichocheo chako, ndivyo utakavyoweza kukikabili mapema zaidi. Kuwa mvumilivu katika kuchunguza na kutambua hisia za mwili wako; wakati mwingine huchukua muda kuunganika na hisia za mwilini.